Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeingia makubaliano na Kampuni ya Clouds plus Production yenye lengo la kushirikiana katika kutafuta rasilimali za uendeshaji wa Tamasha la kimataifa la 38 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo linalotegemewa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano iliyofanyika leo katika ukumbi mkubwa wa maonyesho wa TaSUBa,Mkuu wa Chuo wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye alisema kuwa lengo kuu la makubaliano hayo ni kutafuta rasilimali zitazowezesha kuendesha Tamasha hilo lenye lengo la kuenzi,kudumisha na kutunza Utamaduni wa mtanzania.
Aliongeza kuwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1982 Tamasha limekuwa likifanyika kila mwaka bila kukosa mbali na kukumbwa na uhaba wa pesa za uendeshaji,lakini ana amini kwa kushirikiana na Kampuni kubwa ya biashara ya Clouds Plus Production,tamasha linaweza kuvutia wawekezaji mbalimbali.
Naye mkurugenzi wa uendeshaji wa Clouds Plus Production Bw.Ramadhani Bukini alisema kuwa Kampuni yake inayomiliki Televisheni na Redio itatumia mbinu mbalimbali katika kulitangaza tamasha duniani ili kufanya tamasha hilo lifikie malengo yake ya kuenzi na kudumisha utamaduni wa mtanzania na pia kuvutia wawekezaji wengi.
Hafla hiyo fupi ilisindikizwa na burudani ya Muziki wa asili iliyotolewa na kundi la maonyesho cha Bagamoyo Players kinaloundwa na wakufunzi wa TaSUBa
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.Box 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 023 2440149
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2020 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo . All rights reserved.