• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • NeST |
    • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS)) |
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Huduma Zetu
    • Kikundi cha Bagamoyo
    • Vyumba vya Mikutano
    • Ushauri
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Ofisi
    • Vitengo
  • Taaluma
    • Kozi Zitolewazo
    • Fomu za Maombi
    • Matokeo ya Mtihani
    • Prospectus
  • Tamasha la Bagamoyo
    • Kuhusu Tamasha
    • Mwongozo wa Tamasha
    • Fomu za Maombi ya Tamasha
    • Tamasha la 43
    • Tamasha la 42
    • Tamasha la 41
    • Tamasha la 40
    • Tamasha la 39
    • Tamasha la 38
  • Kituo cha habari
    • TaSUBa TV
    • Maktaba ya Picha
  • Wasiliana
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Majarida
    • Vipeperushi
    • Taarifa kwa umma

*DKT. NDUMBARO - UTANDAWAZI USITUMIKE KUHARIBU UTAMADUNI WETU*

Posted on: September 15th, 2024

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ametoa msisitizo kwa jamii za kitanzania kutumia utandawazi kuongeza maarifa katika kuleta maendeleo badala ya kuacha utandawazi uharibu utamaduni wa Taifa.

Mhe. Ndumbaro ametoa msisitizo huo wakati akifungua Mdahalo wa Kitaifa wa Maadili uliofanyika Septemba 14, 2024  katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ikiwa ni  kuelekea Tamasha la Tatu la Utamaduni la Kitaifa litakalofanyika kuanzia Septemba 20 - 23, 2024 katika uwanja wa Majimaji Songea.

Amesema Tanzania ina mila na desturi zake ambazo ni tofauti na mataifa mengine na kusisitiza kuwa wizara ina muongozo wa maadili katika shughuli za Utamaduni, Sanaa na Michezo ndani na nje ya Tanzania.

"Taifa lisilokuwa na Utamaduni wake ni mfu" haya ni maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Rais wetu wa sasa, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameendelea kutoa msisitizo kwa jamii kufuata mila na desturi za jamii ambapo kupitia maelekezo yake kwa wizara kuwa na Tamasha la Utamaduni kila mwaka kwa mikoa tofauti.

Ameongoza kuwa, utamaduni ndio msingi wa maadili pia ni mfumo wa uongozi, chakula, mavazi, elimu, sherehe, utamaduni usioshikika na unaoshikika.

Aidha, Mhe. Waziri ametoa wito kwa wana Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika Tamasha hilo ambapo mgeni rasmi siku ya kilele Septemba 23, 2024, atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika hatua nyingine, amewasihi wananchi wa Ruvuma kujitokeza kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba mwaka huu.

Awali akimkaribisha Waziri, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni katika wizara hiyo, Bw. Boniface Kadili amesema Mdahalo huo ni sehemu ya utekekezaji wa Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 ambapo amesema sera hiyo inaeleza wajibu wa jamii katika kuenzi, kulinda na kukuza mila na desturi.

Mdahalo huo umeongozwa na mada mbalimbali zikiwemo za athari za mmomonyoko wa maadili kwa maendeleo ya jamii, nafasi ya viongozi wa kisiasa na kijamii katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili pamoja na umuhimu wa maadili kwa maendeleo ya jamii.

Matangazo

  • FOMU YA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2025-2026 SEPTEMBER INTAKE May 28, 2025
  • JOIN INSTRUCTION KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026 April 02, 2025
  • Call for the artists Bagamoyo Festival - 2025 May 05, 2025
  • Wito kwa wasanii Tamasha la Bagamoyo - 2025 May 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KARIBU UJIUNGE NA KOZI YA MUDA MFUPI YA MUZIKI

    May 29, 2025
  • JIUNGE NA CHUO INGIZO LA MACHI 2025

    March 04, 2025
  • JIUNGE NA CHUO INGIZO LA MACHI 2025

    December 19, 2024
  • *SERIKALI KUENDELEA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA TaSUBa*

    December 07, 2024
  • Angalia zote

Video

KARIBU JIUNGE NA CHUO TaSUBa KWA MUHULA WA MACHI 2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS))
  • Dirisha la Hati ya Mshahara
  • Baraza la Sanaa la Taifa

Viunganishi Linganifu

  • WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Kaole Road

    Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania

    Simu: +255 762544613

    Simu ya kiganjani: +255 766 264 581

    Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas

Other Contacts

   

Idadi ya waliotembelea Tovuti

Counter Widgets

    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.