• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • NeST |
    • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS)) |
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Huduma Zetu
    • Kikundi cha Bagamoyo
    • Vyumba vya Mikutano
    • Ushauri
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Ofisi
    • Vitengo
  • Taaluma
    • Kozi Zitolewazo
    • Fomu za Maombi
    • Matokeo ya Mtihani
    • Prospectus
  • Tamasha la Bagamoyo
    • Kuhusu Tamasha
    • Mwongozo wa Tamasha
    • Fomu za Maombi ya Tamasha
    • Tamasha la 43
    • Tamasha la 42
    • Tamasha la 41
    • Tamasha la 40
    • Tamasha la 39
    • Tamasha la 38
  • Kituo cha habari
    • TaSUBa TV
    • Maktaba ya Picha
  • Wasiliana
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Majarida
    • Vipeperushi
    • Taarifa kwa umma

Tamasha la 43

WITO KWA WASANII KUSHIRIKI KATIKATAMASHA LA 43 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYOKUANZIA TAREHE 23 HADI 26 OKTOBA 2024


UTANGULIZI:

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Zamani ikijulikana kama Chuo Cha Sanaa Bagamoyo)inawakaribisha wasanii binafsi na vikundi kutoka sehemu mbalimbali duniani kuomba kushiriki katika Tamashaambalo litakalofanyika katika viwanja na kumbi za Taasisi (TaSUBa - Bagamoyo) kuanzia tarehe 23 hadi 26Oktoba, 2024, katika mji wa kihistoria wa Bagamoyo, Tanzania.


KUHUSU TAMASHA:

Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ni tukio ambalo ni la kipekee na lenye kuvutia sana. Kwakuwa linahusisha na kuchanganya aina mbalimbali za sanaa kama muziki wa asili na kisasa, ngoma, maigizo,sarakasi, vichekesho, mazingaombwe, mashairi, maonyesho (exhibition) na sanaa zingine. Tamasha hili linatoajukwaa la kipekee kwa wasanii wa ndani na kimataifa kushirikiana na kubadilishana uzoefu na ujuzi.


SIFA ZA USHIRIKI:

TaSUBa inawakaribisha wasanii wa fani mbalimbali za sanaa na utamaduni kwa ajili ya kuomba kushiriki katikaTamasha. Iwe wewe ni mwimbaji, mwanamuziki, mchekeshaji, msanii wa sanaa za ufundi (mchoraji, mchongasanamu), au mtaalamu mwingine wa ubunifu, tunakaribisha maombi yako ya kushiriki katika Tamasha.


JINSI YA KUOMBA:

 Tembelea Tovuti yetu: Tembelea tovuti ya TaSUBa www.tasuba.ac.tz kupata habari za kina kuhusuTamasha, ikiwa ni pamoja na mchakato wa maombi, na miongozo ya Tamasha.MKUU WA CHUO, TaSUBa, S.L.P 32, BAGAMOYO, Tanzania, Simu: +255(0) 023 2440032Namba za Simu: +255(0) 755 853 436, +255(0) 714 510 386, and +255(0) 788 840 405Barua Pepe: bagamoyofest@tasuba.ac.tz au bagamoyofest@gmail.comTovuti: www.tasuba.ac.tz

 Jaza Fomu ya Maombi: Nenda kwenye sehemu ya "Tamasha" kwenye tovuti na upakue fomu ya maombi.Jaza kwa usahihi kuhusu taarifa Msanii/Kikundi na maelezo mengine.

 Mwisho wa Maombi: Mwisho wa kuwasilisha maombi ya kushiriki Tamasha ni Julai 31, 2024.


UTARATIBU WA MAOMBI YA USHIRIKI:

Ili kupata nafasi ya ushiriki, tafadhali wasilisha yafuatayo:

 Fomu kamili ya Maombi:

 Maelezo ya Msanii: Maelezo mafupi kuhusu Msanii/Kikundi (Artist Biography).

 Wasilisha kazi yako: Ambatanisha picha au video fupi za kazi zako au viungo (links) kwenye portfolia aumaonyesho ya mtandaoni yanayoonyesha mtindo wako wa sanaa.


MCHAKATO WA MCHUJO:

Kamati ya Tamasha itapitia kwa makini maombi yote na kuchagua wasanii/vikundi ambao kazi zao zitaonekanakuendana na malengo na mandhari ya Tamasha. Wasanii wote watakaopata na kukosa nafasi ya kufanya onyeshowatapewa taarifa ifikapo Agosti 31, 2024.


FAIDA KWA WASANII WATAKAOCHAGULIWA:

i. Kukutana na kufanya onyesho katika hadhira kubwa yenye mchanganyiko tofauti.

ii. Fursa za kujenga mtandao na wasanii wengine na wadau wa sanaa na utamaduni.


Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana

Barua pepe: bagamoyofest@tasuba.ac.tz au bagamoyofest@gmail.com

Tovuti: www.tasuba.ac.tz

Simu: +255(0) 755 853 436, +255(0) 714 510 386, na +255(0) 788 840 405

Ili kupakuwa fomu ya Tamasha la 43 bonyeza link hapo chini:

FOMU YA USHIRIKI WA TAMASHA - 2024.pdf


Matangazo

  • FOMU YA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2025-2026 SEPTEMBER INTAKE May 28, 2025
  • JOIN INSTRUCTION KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026 April 02, 2025
  • Call for the artists Bagamoyo Festival - 2025 May 05, 2025
  • Wito kwa wasanii Tamasha la Bagamoyo - 2025 May 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KARIBU UJIUNGE NA KOZI YA MUDA MFUPI YA MUZIKI

    May 29, 2025
  • JIUNGE NA CHUO INGIZO LA MACHI 2025

    March 04, 2025
  • JIUNGE NA CHUO INGIZO LA MACHI 2025

    December 19, 2024
  • *SERIKALI KUENDELEA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA TaSUBa*

    December 07, 2024
  • Angalia zote

Video

KARIBU JIUNGE NA CHUO TaSUBa KWA MUHULA WA MACHI 2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS))
  • Dirisha la Hati ya Mshahara
  • Baraza la Sanaa la Taifa

Viunganishi Linganifu

  • WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Kaole Road

    Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania

    Simu: +255 762544613

    Simu ya kiganjani: +255 766 264 581

    Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas

Other Contacts

   

Idadi ya waliotembelea Tovuti

Counter Widgets

    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.