• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • NeST |
    • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS)) |
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Huduma Zetu
    • Kikundi cha Bagamoyo
    • Vyumba vya Mikutano
    • Ushauri
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Ofisi
    • Vitengo
  • Taaluma
    • Kozi Zitolewazo
    • Fomu za Maombi
    • Matokeo ya Mtihani
    • Prospectus
  • Tamasha la Bagamoyo
    • Kuhusu Tamasha
    • Mwongozo wa Tamasha
    • Fomu za Maombi ya Tamasha
    • Tamasha la 43
    • Tamasha la 42
    • Tamasha la 41
    • Tamasha la 40
    • Tamasha la 39
    • Tamasha la 38
  • Kituo cha habari
    • TaSUBa TV
    • Maktaba ya Picha
  • Wasiliana
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Majarida
    • Vipeperushi
    • Taarifa kwa umma

*TAMASHA LA KIMATAIFA LA BAGAMOYO LAINUA UCHUMI WA BAGAMOYO*

Posted on: October 27th, 2024

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa amesema Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ni bidhaa ya kiuchumi kwa wakazi wa mji huo na amewataka kulitumia kwa kukuza uchumi wao na kuitangaza Bagamoyo.

Msigwa ameyasema hayo Oktoba 26, 2024 alipokuwa mgeni rasmi wakati wa kilele cha Tamasha hilo lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.

Msigwa amewataka wakazi wa Bagamoyo na maeneo ya jirani kutanua huduma za makazi, chakula, mavazi, malazi, usafiri, bidhaa za kitamaduni na sanaa ili kukidhi mahitaji ya wageni na washiriki wa Tamasha hilo kubwa linalofanyika kila mwaka.

Katika hatua nyingine, Msigwa amesema kuwa Wizara itaongeza bajeti ya Tamasha la 44 mwakani ili kutimiza lengo la kufanyika kwa siku saba huku akiagiza kuwa na wasanii wakubwa wa kutumbuiza kwa siku zote za tamasha.

Naye Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Herbert Makoye amewashukuru washiriki na wananchi wote waliojitokeza kuhudhuria shughuli hiyo na kuwaahidi kuboresha zaidi katika Tamasha linalofuata la mwakani.

Tamasha hili la Sanaa na Utamaduni, hufanyika kila mwaka katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ambapo hukutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Tamasha hili hulenga kukuza vipaji, kuuenzi na kuutunza na kurithisha Utamaduni wetu kwa vizazi vijavyo, kutangaza utalii wa mji wa Bagamoyo, pia kutoa ajira kwa wasanii wa nyanja mbalimbali nchini.

Matangazo

  • FOMU YA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2025-2026 SEPTEMBER INTAKE May 28, 2025
  • JOIN INSTRUCTION KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026 April 02, 2025
  • Call for the artists Bagamoyo Festival - 2025 May 05, 2025
  • Wito kwa wasanii Tamasha la Bagamoyo - 2025 May 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KARIBU UJIUNGE NA KOZI YA MUDA MFUPI YA MUZIKI

    May 29, 2025
  • JIUNGE NA CHUO INGIZO LA MACHI 2025

    March 04, 2025
  • JIUNGE NA CHUO INGIZO LA MACHI 2025

    December 19, 2024
  • *SERIKALI KUENDELEA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA TaSUBa*

    December 07, 2024
  • Angalia zote

Video

KARIBU JIUNGE NA CHUO TaSUBa KWA MUHULA WA MACHI 2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS))
  • Dirisha la Hati ya Mshahara
  • Baraza la Sanaa la Taifa

Viunganishi Linganifu

  • WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Kaole Road

    Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania

    Simu: +255 762544613

    Simu ya kiganjani: +255 766 264 581

    Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas

Other Contacts

   

Idadi ya waliotembelea Tovuti

Counter Widgets

    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.