• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • NeST |
    • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS)) |
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Huduma Zetu
    • Kikundi cha Bagamoyo
    • Vyumba vya Mikutano
    • Ushauri
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Ofisi
    • Vitengo
  • Taaluma
    • Kozi Zitolewazo
    • Fomu za Maombi
    • Matokeo ya Mtihani
    • Prospectus
  • Tamasha la Bagamoyo
    • Kuhusu Tamasha
    • Mwongozo wa Tamasha
    • Fomu za Maombi ya Tamasha
    • Tamasha la 43
    • Tamasha la 42
    • Tamasha la 41
    • Tamasha la 40
    • Tamasha la 39
    • Tamasha la 38
  • Kituo cha habari
    • TaSUBa TV
    • Maktaba ya Picha
  • Wasiliana
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Majarida
    • Vipeperushi
    • Taarifa kwa umma

TaSUBa YAINGIA MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA (TBC)

Posted on: June 19th, 2021

TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeingia makubaliano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ili kukuza, kuboresha na kutangaza Sanaa na Utamaduni wa mtanzania.

Akizungumza jana mjini Dodoma mara baada ya kusaini makubaliano hayo Hafla ya utiaji saini huo, imefanyika Dodoma tarehe 19 Juni, 2021 katika  ofisi za TBC,Mkuu wa TaSUBa Dk. Herbert Makoye, alisema makubaliano hayo yataisaidia taasisi hiyo  kutengeneza maudhui katika maeneo wanayoshughulikia.

Dk. Makoye alisema kupitia makubaliano hayo TBC watatengeneza vipindi vya runinga  kwa njia ya tamthilia, hatua ambayo ni muhimu katika kufikisha ujumbe kwa wananchi.

Alisema kutengeneza tamthilia ni njia nzuri yakutangaza lugha  ya Kiswahili na Utamaduni wa mtanzania.

Dk. Makoye aliongeza kuwa utengenezaji wa tamthilia utaisaidia TaSUBa kuonyesha kazi wanazofanya na mchango katika taifa na utamaduni.

"TaSUBa ina malengo ya kusaidia utamaduni  wa mtanzania uvuke mipaka kwa kutumia vyombo vya habari vyenye nguvu ili kuzifikia ncho jirani  wasifikiri sisi ni wa kupokea tu tamaduni zao"alisema.

Aidha, makubaliano hayo yatawapa nafasi wanafunzi TaSUBa kufanya mazoezi kwa vitendo wakiwa na uhitaji  huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TBC Dk.Ayoub Rioba alimshukuru Mkuu wa TaSUBa kufuatia makubaliano hayo.

“TBC dhima yetu ni kuhakikisha kwamba tunaendeleza na kudumisha Utamaduni, kwa sababu utamaduni kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwa ni vyenzo muhimu  katika kumuendeleza binadamu, taifa lisilo na utamaduni ni sawa na lililokufa” alisema.

Dk. Rioba alisema TBC wanatambua   mchango wa TaSUBa katika kuendeleza utamaduni wa mtanzania.

Dkt. Rioba alisisitiza, “baada ya kusaini makubaliano haya kazi ya kuanza kuandaa kazi kazi za Sanaa itaanza mara moja ili zianze kuruka katika vyombo vyetu ambavyo ni redio, televisheni ambayo inaweza ikawa ni TBC1, TBC 2 na mitandao ya kijamii.”alisema.

Aidha Dk. Rioba aliongeza kuwa anaamini nia waliyonayo TaSUBa na TBC ni ya dhati na wote tunapenda kuona tunaendeleza Utamaduni wetu.

Matangazo

  • FOMU YA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2025-2026 SEPTEMBER INTAKE May 28, 2025
  • JOIN INSTRUCTION KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026 April 02, 2025
  • Call for the artists Bagamoyo Festival - 2025 May 05, 2025
  • Wito kwa wasanii Tamasha la Bagamoyo - 2025 May 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KARIBU UJIUNGE NA KOZI YA MUDA MFUPI YA MUZIKI

    May 29, 2025
  • JIUNGE NA CHUO INGIZO LA MACHI 2025

    March 04, 2025
  • JIUNGE NA CHUO INGIZO LA MACHI 2025

    December 19, 2024
  • *SERIKALI KUENDELEA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA TaSUBa*

    December 07, 2024
  • Angalia zote

Video

KARIBU JIUNGE NA CHUO TaSUBa KWA MUHULA WA MACHI 2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS))
  • Dirisha la Hati ya Mshahara
  • Baraza la Sanaa la Taifa

Viunganishi Linganifu

  • WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Kaole Road

    Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania

    Simu: +255 762544613

    Simu ya kiganjani: +255 766 264 581

    Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas

Other Contacts

   

Idadi ya waliotembelea Tovuti

Counter Widgets

    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.