• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • NeST |
    • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS)) |
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Huduma Zetu
    • Kikundi cha Bagamoyo
    • Vyumba vya Mikutano
    • Ushauri
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Ofisi
    • Vitengo
  • Taaluma
    • Kozi Zitolewazo
    • Fomu za Maombi
    • Matokeo ya Mtihani
    • Prospectus
  • Tamasha la Bagamoyo
    • Kuhusu Tamasha
    • Mwongozo wa Tamasha
    • Fomu za Maombi ya Tamasha
    • Tamasha la 43
    • Tamasha la 42
    • Tamasha la 41
    • Tamasha la 40
    • Tamasha la 39
    • Tamasha la 38
  • Kituo cha habari
    • TaSUBa TV
    • Maktaba ya Picha
  • Wasiliana
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Majarida
    • Vipeperushi
    • Taarifa kwa umma

WANAFUNZI CHUO CHA TAALUMA YA UREKEBISHAJI TANZANIA (TCTA) WATEMBELEA TaSUBa

Posted on: May 26th, 2022




Wanafunzi katoka Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) wakiambatana na Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo hicho, Taaluma, Utafiti na Ushauri pamoja na wakufunzi, wametembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Mei 25, 2022 ikiwa ni ziara ya kimasomo ili kutimiza matakwa ya makubaliano (MoU) kati ya vyuo hivyo viwili. 


Katika ziara hiyo Kaimu Mkuu wa  chuo TaSUBa, ambaye ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Mwl. Gabriel Kiiza alisema, makubaliano ambayo TaSUBa iliingia na TCTA yanahusisha utoaji wa mafunzo  kwa kipindi cha muda mfupi kisichopungua mwezi mmoja na kisichozidi miezi mitatu kwa kila udhahili.


Mwl. Kiiza alisema, tasnia ya sanaa na utamaduni inahitaji ubunifu ili kuiboresha na kuleta vitu vipya kila wakati, ambapo mbali na kuwa ni burudani, ni sehemu ya ajira rasmi ambayo inahusisha kundi kubwa la vijana ambao ni nguvu kazi katika uchumi endelevu.


Kwa upande wake Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo TCTA  Mrakibu wa Magereza  Lihuwi Said Ngonya, alisema makubaliano hayo yamekuwa na tija kwa wanafunzi wa TCTA kwani wamepata na fursa ya kutembelea TaSUBa na kujifunza mengi.


Mrakibu Ngonya alisema, ushirikiano huo  ni fursa nzuri ya kupeana uzoefu katika  Sanaa na Utamaduni kwa kuwa TaSUBa wamebobea na wana uzoefu katika utoaji wa mafunzo hayo.


Makubaliano hayo kati ya TaSUBa na TCTA yanahitaji wanafunzi kutoka TCTA kutembelea TaSUBa  ili  kujifunza mazingira ya Taasisi hiyo kabla ya kuhitimu mafunzo angalau mara moja kwa kila udhahili.





Matangazo

  • FOMU YA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2025-2026 SEPTEMBER INTAKE May 28, 2025
  • JOIN INSTRUCTION KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026 April 02, 2025
  • Call for the artists Bagamoyo Festival - 2025 May 05, 2025
  • Wito kwa wasanii Tamasha la Bagamoyo - 2025 May 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KARIBU UJIUNGE NA KOZI YA MUDA MFUPI YA MUZIKI

    May 29, 2025
  • JIUNGE NA CHUO INGIZO LA MACHI 2025

    March 04, 2025
  • JIUNGE NA CHUO INGIZO LA MACHI 2025

    December 19, 2024
  • *SERIKALI KUENDELEA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA TaSUBa*

    December 07, 2024
  • Angalia zote

Video

KARIBU JIUNGE NA CHUO TaSUBa KWA MUHULA WA MACHI 2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS))
  • Dirisha la Hati ya Mshahara
  • Baraza la Sanaa la Taifa

Viunganishi Linganifu

  • WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Kaole Road

    Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania

    Simu: +255 762544613

    Simu ya kiganjani: +255 766 264 581

    Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas

Other Contacts

   

Idadi ya waliotembelea Tovuti

Counter Widgets

    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.