Tuesday 23rd, June 2026
@TaSUBa Bagamoyo
WITO KWA WASANII KUSHIRIKI KATIKATAMASHA LA 44 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYOKUANZIA TAREHE 28 HADI 31 OKTOBA 2026
UTANGULIZI:
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Zamani ikijulikana kama Chuo Cha Sanaa Bagamoyo)inawakaribisha wasanii binafsi na vikundi kutoka sehemu mbalimbali duniani kuomba kushiriki katika Tamashaambalo litakalofanyika katika viwanja na kumbi za Taasisi (TaSUBa - Bagamoyo) kuanzia tarehe 28 hadi 31 Oktoba, 2026, katika mji wa kihistoria wa Bagamoyo, Tanzania.
KUHUSU TAMASHA:
Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ni tukio ambalo ni la kipekee na lenye kuvutia sana. Kwakuwa linahusisha na kuchanganya aina mbalimbali za sanaa kama muziki wa asili na kisasa, ngoma, maigizo,sarakasi, vichekesho, mazingaombwe, mashairi, maonyesho (exhibition) na sanaa zingine. Tamasha hili linatoajukwaa la kipekee kwa wasanii wa ndani na kimataifa kushirikiana na kubadilishana uzoefu na ujuzi.
SIFA ZA USHIRIKI:
TaSUBa inawakaribisha wasanii wa fani mbalimbali za sanaa na utamaduni kwa ajili ya kuomba kushiriki katikaTamasha. Iwe wewe ni mwimbaji, mwanamuziki, mchekeshaji, msanii wa sanaa za ufundi (mchoraji, mchongasanamu), au mtaalamu mwingine wa ubunifu, tunakaribisha maombi yako ya kushiriki katika Tamasha.
JINSI YA KUOMBA:
CLICK THE LINK BELOW TO FILL IN THE FORM
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.