Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba katika mji mkongwe na wa kihostoria wa Bagamoyo - mji wenye historia adhimu na vivutio lukuki vya urithi wa utamaduni wa Mtanzania vinavyotambuliwa na Shirika la UNESCO. Tamasha hili huandaliwa na kuendeshwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa); Taasisi inayotoa mafunzo ya sanaa na utamaduni kwa vijana wenye vipaji. Wakati wote wa Tamasha, maeneo yote ya TaSUBa hupambwa na kazi za sanaa na maonesho mbalimbali ya sanaa. Wasanii mahiri kutoka sehemu mbalimbali za Dunia ambao hufika kuonesha kazi zao za ubunifu wa hali ya juu. Aidha, Tamasha hili huvutia watazamaji, wadau na wapenzi wa sanaa kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje yaTanzania.
Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo lilianza mwaka 1981 kwa kushirikisha kazi za sanaa za wanafunzi na walimu wa TaSUBa pekee. Hata hivyo limeendelea kukua na kuwa maarufu sana na kuchukua sura ya Kitaifa kiasi cha kuwavutia watazamaji na wasanii wengi kutoka mataifa mbalimbali, hivyo kulifanya liwe la Kimataifa zaidi. Zaidi ya vikundi vya sanaa/ wasanii 1,500 wamepata nafasi ya kushiriki kwenye Tamasha hili tangu lianze; kati ya hawa, vikundi vya sanaa/ wasanii 1,300 wakiwa ni wa ndani na 200 ni kutoka nchi mbalimbali. Tamasha hili pia limekuwa kivutio kikubwa kwa watazamaji vijana kutoka katika shule na vyuo mbalimbali vya hapa nchini.
Lengo kuu la Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo ni kutoa nafasi kwa wasanii wa ndani ya nchi na wale kutoka nje kukutana na kusherehekea uanuai wa utamaduni unaochagiza mshikamano na bunifu mbalimbali. Malengo mahsusi ya Tamasha ni haya yafuatayo:
Mbali na kukusanya wasanii maarufu wa ndani na nje, Tamasha hili hutoa nafasi ya kuonyesha sanaa za ufundi na vifaa vingine vya kiutamaduni, vyakula vya asili, kutembelea vivutio vya kitalii nchini Tanzania, michezo ya watoto na mafunzo mafupi mafupi ya utengenezaji au uandaaji wa sanaa.
Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo huandaliwa na:
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
Barabara ya Kaole, S. L. P 32, Bagamoyo, Tanzanaia
Barua Pepe: info@tasuba.ac.tz/ tasuba@michezo.go.tz Wavuti: www.tasuba.ac.tz
Kuhusu Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo.p.pdf
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.