• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • NeST |
    • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS)) |
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Huduma Zetu
    • Kikundi cha Bagamoyo
    • Vyumba vya Mikutano
    • Ushauri
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Ofisi
    • Vitengo
  • Taaluma
    • Kozi Zitolewazo
    • Fomu za Maombi
    • Matokeo ya Mtihani
    • Prospectus
  • Tamasha la Bagamoyo
    • Tamasha la 44
    • Tamasha la 43
    • Tamasha la 42
    • Tamasha la 41
    • Tamasha la 40
    • Tamasha la 39
    • Tamasha la 38
  • Kituo cha habari
    • TaSUBa TV
    • Maktaba ya Picha
  • Wasiliana
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Majarida
    • Vipeperushi
    • Taarifa kwa umma

WASANII WA KOMBOLELA WAWAPIGA MSASA WANACHUO WA TaSUBa

Posted on: February 5th, 2026

BAADHI ya wasanii wa timu ya waigizaji wa Tamthilia ya Kombolela wametembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa lengo la kuwapa wanafunzi uzoefu kwa vitendo kuhusu kazi za sanaa nje ya mazingira ya darasani.


Akizungumza katika ziara hiyo iliyofanyika Februari 05, 2026, Mkuu wa Chuo Dkt. Herbert Makoye amesema ziara ya wasanii hao ni sehemu ya mikakati ya TaSUBa ya kuwajengea wanafunzi uwezo wa ubunifu na umahiri wa kitaaluma ili kuandaa wasanii wanaoweza kujiajiri na kuchangia maendeleo ya nchi yao kupitia kazi za sanaa.


"TaSUBa itaendelea kushirikiana na wasanii wenye uzoefu katika tasnia hii ya sanaa ili kuimarisha mafunzo yanayozingatia weledi kwa vitendo katika kuwapika vijana na kutoa wasanii bora," amesema Dkt. Makoye.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bw. Lumole Matovolwa ambae ni mmoja wa wasanii wa Timu Kombolela amesema sanaa ina mchango mkubwa katika kufikisha ujumbe kwa jamii moja kwa moja, hususan katika masuala ya kijamii kama afya, elimu, uwajibikaji, mazingira na mshikamano katika jamii.


"Kupitia sanaa hii jamii hujifunza kwa njia rahisi na yenye kuvutia kwa kuwa inakua ni sehemu ya burudani," amesema Matovolwa.


Akiongea kwa ni niaba ya wakufunzi wa TaSUBa Bi. Beatrice Taisamo amesema ziara hiyo ni muhimu kwa wanafunzi kwani imewawezesha kujifunza kwa vitendo nje ya mazingira ya darasani na kuelewa uhalisia wa kazi ya sanaa katika jamii.


Naye mmoja wa wanafunzi wa TaSUBa Bi. Faraja Ibrahimu amesema ziara hiyo imewapanua mawazo na kuwajengea ujasiri wa kutumia sanaa kama chombo cha kuelimisha na kuhamasisha jamii.

Matangazo

  • MAELEKEZO YA KUJIUNGA TaSUBa MWAKA 2026/2027 INGIZO LA MWEZI MACHI March 31, 2026
  • SELECTED APPLICANTS MARCH INTAKE 2026 March 31, 2026
  • WITO KWA WASANII MPYA July 21, 2025
  • FOMU YA USHIRIKI WA TAMASHA MPYA July 21, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KARIBU UJIUNGE NA CHUO MWAKA WA MASOMO 2026/2027

    April 30, 2026
  • KARIBU UJIUNGE NA CHUO MWAKA WA MASOMO 2026/2027

    April 23, 2026
  • KARIBU UJIUNGE NA CHUO MWAKA WA MASOMO 2026/2027

    April 22, 2026
  • WASANII WA KOMBOLELA WAWAPIGA MSASA WANACHUO WA TaSUBa

    February 05, 2026
  • Angalia zote

Video

Je, unakidhi sifa za kujiunga TaSUBa?
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS))
  • Dirisha la Hati ya Mshahara
  • Baraza la Sanaa la Taifa

Viunganishi Linganifu

  • WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Kaole Road

    Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania

    Simu: +255 762544613

    Simu ya kiganjani: +255 766 264 581

    Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas

Other Contacts

   

Idadi ya waliotembelea Tovuti

Counter Widgets

    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.