TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)ni zao la kilichokuwa Chuo cha Sanaa Bagamoyo. Historia ya ya chuo cha Sanaa Bagamoyo ilianzia mnamo mwaka 1962 ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanganyika iliundwa wizara ya vijana na utamaduni. Mnamo mwaka 1972 ilionekana kuwa kuna uhitaji wa kuwa na mafunzo rasmi ya mambo ya Sanaa, hii ilipelekea kuanzishwa kwa chuo cha sanaa Bagamoyo(BCA). Kati ya mwaka 2003-2005 Chuo cha Sanaa Bagamoyo kilisajiliwa na Baraza la taifa la elimu ya ufundi (NACTE), na kuanzia hapo mitaala ya kufundishia iliandaliwa kikamilifu na kupata ithibati ya NACTE. Mwishoni mwa mwaka 2005 uamuzi ulifanywa na iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni kwamba, Chuo cha Sanaa Bagamoyo kibadilishwe kuwa wakala wa Serikali chini ya mpango wa mabadiliko ya sekta ya umma,kwa hiyo Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ilianzishwa mnamo tarehe 2 Novemba 2007, kwa tangazo namba 220 lililochapishwa kwenye gazeti la Serikali kwa mujibu wa sheria ya Wakala wa Serikali namba 30 ya mwaka 1997.
Taasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo ni kituo chenye ubora uliotukuka Afrika Mashariki katika kutoa mafunzo ya Sanaa za maonyesho na ufundi ambapo majukumu yake makubwa ni kuhudumia mahitaji ya nchi washirika wa jumuiya ya Afrika Mashariki katika kutunza, kuhamasisha na kuendeleza Sanaa za maonyesho na ufundi.
MAJUKUMU YA TaSUBa
Kutoa mafunzo
Kufanya utafiti katika masuala yanayohusu Sanaa na Utamaduni
Kutoa ushauri katika masuala yanayohusu Sanaa na Utamaduni
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.