VIJANA wasanii wametakiwa kutafahamu kuwa wana nafasi kubwa katika kulinda na kuimarisha amani ya nchi kupitia kazi zao za sanaa za muziki, ngoma, filamu, maigizo, uchoraji au fasihi.
Hayo yamesemwa leo Desemba 19, 2025 na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamisi Mwinjuma katika Mahafali ya 36 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
Mhe. Waziri ambaye alikua Mgeni Rasmi katika mahafali hayo amewataka wasanii kutambua kuwa sanaa yao inaweza kuwa chombo muhimu katika kuelimisha jamii, kupunguza migogoro, kujenga maelewano na kuhimiza uzalendo.
"Epukeni kutumia sanaa au majukwaa ya mitandao ya kijamii kuchochea chuki, migawanyiko au vurugu. Badala yake, tumieni vipaji vyenu kuhubiri amani, umoja na mshikamano wa kitaifa," amesema Mhe. Waziri.
Mhe. Mwinjuma amewata wahitimu wote kuwa walinzi wa amani ya Taifa letu, mabalozi wa maadili mema na chachu ya maendeleo chanya katika jamii.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.