WANAFUNZI na watumishi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) leo wameshiriki mazoezi ya yoga yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya 12 ya Kimataifa ya Yoga yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.Mazoezi hayo yaliandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Watu wa India kwa lengo la kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa yoga katika kuimarisha afya ya mwili, akili na ustawi wa maisha kwa ujumla.Washiriki walipata fursa ya kujifunza na kufanya mazoezi mbalimbali ya yoga chini ya uongozi wa wataalamu, huku wakielezwa manufaa ya yoga katika kupunguza msongo wa mawazo, kuongeza umakini na kuboresha afya ya mwili.Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, mmoja wa waandaaji alieleza kuwa yoga ni nyenzo muhimu ya kujenga afya bora na kuimarisha mahusiano ya kijamii kupitia mazoezi yanayowaleta watu pamoja bila kujali tofauti zao.Kwa upande wake, TaSUBa imeendelea kuonesha ushirikiano wake katika shughuli zinazochangia maendeleo ya sanaa, utamaduni na ustawi wa jamii kwa kushiriki kikamilifu katika mazoezi hayo. Ushiriki huo pia umeonesha dhamira ya taasisi katika kuhamasisha mtindo bora wa maisha unaojumuisha afya ya mwili na akili.Maadhimisho ya Kimataifa ya Yoga huadhimishwa duniani kote kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya yoga kama njia ya kuimarisha afya, amani na mshikamano miongoni mwa watu wa mataifa mbalimbali.
Mhitimu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Karim Swafi, ameendelea kuonyesha uwezo mkubwa wa vijana wa Kitanzania katika medani za kimataifa baada ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano ya Yogasana yaliyofanyika jijini Ahmedabad, India, na kufanikiwa kujishindia tuzo nne.Mafanikio hayo yameiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa ya mchezo na sanaa ya Yogasana, huku yakionesha matokeo chanya ya uwekezaji katika elimu ya sanaa na maendeleo ya vipaji vya vijana. Karim alionesha umahiri, nidhamu na ubunifu wa hali ya juu katika mashindano hayo yaliyowakutanisha washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani.Mafanikio ya Karim Swafi yanaendelea kuthibitisha kuwa TaSUBa ni kitovu cha kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vinavyoweza kushindana na kufanya vizuri katika ngazi za kitaifa na kimataifa.
Katika ulimwengu wa muziki unaoendelea kukua kwa kasi, hitaji la wataalamu wenye ujuzi wa utayarishaji wa muziki wa kisasa limeongezeka zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kinaendelea kuwa kitovu cha kuibua vipaji na kuzalisha wataalamu wa muziki wanaoweza kushindana katika soko la ajira na tasnia ya ubunifu ndani na nje ya Tanzania.Kupitia mafunzo ya kitaalamu yanayojumuisha matumizi ya teknolojia za kisasa za sauti, utayarishaji wa muziki, uandishi wa nyimbo, pamoja na mbinu mbalimbali za uzalishaji wa kazi za muziki, wanafunzi hupata maarifa na ujuzi unaowajengea msingi imara wa mafanikio katika sekta ya muziki.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.