NGUVU YA SANAA KATIKA DUNIA YA TEKNOLOJIA NA UBUNIFU
Kikundi cha dance kinachofahamika kwa jina la Muda Africa kimeonyesha uwezo mkubwa wa kisanaa kwa kuonesha uchezaji wa dansi unaojulikana kama "Frozen Dance" uliowavutia na kuwaacha watazamaji vinywa wazi!Wanakikundi hao walionesha ubunifu, umakini na ushirikiano wa hali ya juu kwa kufanya miondoko iliyokuwa ikisimama ghafla kama sanamu na kisha kuendelea kwa ustadi mkubwa. Umahiri huo uliwafanya watazamaji kufurahia burudani hiyo huku wakitoa makofi na shangwe za pongezi.Maonesho haya yameendelea kuthibitisha kuwa sanaa ya dansi ni jukwaa muhimu la kuonesha vipaji, ubunifu na uwezo wa wasanii wa Tanzania katika kutoa burudani yenye mvuto kwa jamii.
"Vipaji huzaliwa, lakini wasanii huandaliwa. Karibu TaSUBa kwa mwaka wa masomo 2026/2027 ujifunze, ubobe na ufanikiwe katika dunia ya sanaa na utamaduni."
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.