Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Edward Buganga amesema TaSUBa Awards ni mfano wa kuigwa na taasisi nyingine za elimu nchini kwa namna zinavyotambua na kuthamini juhudi za wanafunzi kupitia utoaji wa tuzo.Bw. Buganga alitoa kauli hiyo alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya tuzo za TaSUBa Awards Msimu wa Tatu iliyofanyika Chuoni hapo usiku wa Juni 26, 2026.Amesema kuwa utoaji wa tuzo kwa wanafunzi wenye kufanya vizuri katika taaluma na vipaji ni njia bora ya kuwahamasisha ili kuongeza bidii, ubunifu na ushindani wenye tija, jambo ambalo linachangia kuzalisha wataalamu mahiri wa sekta ya sanaa na utamaduni."TaSUBa imeonyesha mfano mzuri wa kuthamini mafanikio ya wanafunzi wake. Huu ni utaratibu ambao taasisi nyingine za elimu zinaweza kuiga ili kuwajengea wanafunzi ari ya kufanya vizuri zaidi katika masomo na vipaji vyao," amesema Bw. Buganga.Aidha, aliipongeza TaSUBa kwa kuendelea kuandaa TaSUBa Awards kila mwaka, akieleza kuwa hafla hiyo si tu inatambua mafanikio ya wanafunzi bali pia inajenga utamaduni wa kuthamini ubora na kuhamasisha kizazi kipya cha wasanii kufanya kazi kwa weledi.TaSUBa Awards Msimu wa Tatu zimewakutanisha viongozi wa serikali, wadau wa sanaa, wakufunzi, wanafunzi na wageni mbalimbali kushuhudia utoaji wa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika ubunifu na shughuli mbalimbali za kisanaa.Hafla hiyo imeendelea kudhihirisha dhamira ya TaSUBa ya kuendeleza vipaji, kukuza ubora wa elimu ya sanaa na kuandaa wataalamu wenye uwezo wa kushindana katika sekta ya ubunifu nchini na kimataifa.
Mkuu wa Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye, amesema kuwa TaSUBa Awards zimeanzishwa kwa lengo la kuwapa hamasa wanachuo ili wafanye vizuri zaidi katika masomo yao na kuendeleza vipaji vyao vya kisanii.Akizungumza kuelekea msimu wa tatu wa TaSUBa Awards, Dkt. Makoye alisema tuzo hizo ni sehemu ya kutambua juhudi, ubunifu na mafanikio ya wanafunzi katika nyanja mbalimbali za sanaa na utamaduni.“TaSUBa Awards ni tuzo zinazotoa hamasa kwa wanachuo wetu ili waweze kufanya vizuri zaidi na kuweka jitihada katika masomo na vipaji vyao kwa ujumla. Tunapenda kuona tuzo hizi zikiendelea kukua na kuwa kubwa zaidi kila mwaka,” amesema Dkt. Makoye.Aliongeza kuwa TaSUBa itaendelea kuboresha mfumo wa tuzo hizo ili ziwe chachu ya ushindani wenye tija, ubunifu na maendeleo ya tasnia ya sanaa nchini.TaSUBa Awards zimeendelea kuwa moja ya matukio muhimu chuoni, zikitoa fursa ya kutambua na kuthamini vipaji vya wanafunzi pamoja na kuwahamasisha kuendelea kujifunza, kubuni na kufanya kazi kwa weledi katika sekta ya sanaa na utamaduni.
Kipaji cha kuchora ni zawadi kutoka kwa Mungu, lakini mafanikio katika sanaa yanategemea jitihada za mtu mwenyewe. Kipaji pekee hakitoshi; kinahitaji kuendelezwa kupitia mazoezi ya mara kwa mara, kujifunza mbinu mpya na kujituma kila siku.Elimu ya sanaa ina nafasi kubwa katika kumjenga msanii. Kupitia mafunzo rasmi, mwanafunzi hupata maarifa, mbinu za kisasa na mwongozo kutoka kwa wataalamu wenye uzoefu.Jiunge na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na upate fursa ya kukuza kipaji chako cha uchoraji chini ya wataalamu wa sanaa. TaSUBa ni mahali sahihi ambapo vipaji hukuzwa, ubunifu huimarishwa na ndoto za wasanii hutimia.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.