WITO KWA WASANII KUSHIRIKI KATIKA
TAMASHA LA 42 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO
KUANZIA TAREHE 26 HADI 28 OKTOBA 2023
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo_TaSUBa (Zamani Chuo Cha Sanaa Bagamoyo) inapenda kuwakaribisha wasanii na vikundi vya sanaa kwa ujumla kuomba kushiriki kwa kufanya maonyesho katika Tamasha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo litafanyika katika viwanja vya Taasisi (TaSUBa – Bagamoyo) kuanzia tarehe 26 hadi 28 Oktoba, 2023.
Tamasha hili limekuwa na malengo mbalimbali ikiwemo kuendeleza na kudumisha utamaduni wa Mtanzania, kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka kwa wasanii na vikundi vya ndani na nje ya Tanzania kupitia warsha na maonyesho mbalimbali.
Tamasha hili hujumuisha aina mbalimbali za sanaa kama vile Ngoma, Maigizo, Muziki, Sarakasi, Mazingaombwe, Vichekesho, Filamu pamoja na maonyesho ya sanaa za ufundi (Exhibitions).
TaSUBa inawakaribisha wasanii na vikundi vya sanaa kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya nchi ili kuweza kushiriki katika Tamasha hili kongwe la sanaa na utamaduni wa Mtanzania.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia;
Barua pepe: bagamoyofest@gmail.com au bagamoyofest@tasuba.ac.tz
Tovuti: www.tasuba.ac.tz
Simu: +255(0) 763 408 792, +255(0) 655 840 405, na +255(0) 713 756 168
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.Box 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 023 2440149
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2022 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.