WITO KWA WASANII KUSHIRIKI KATIKATAMASHA LA 44 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYOKUANZIA TAREHE 26 HADI 29 NOVEMBA 2025
UTANGULIZI:
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (Zamani ikijulikana kama Chuo Cha Sanaa Bagamoyo) inawakaribisha wasanii binafsi na vikundi kutoka sehemu mbalimbali duniani kuomba kushiriki katika Tamasha ambalo litakalofanyika katika viwanja na kumbi za Taasisi (TaSUBa - Bagamoyo) kuanzia tarehe 26 hadi 29 Novemba 2025, katika mji wa kihistoria wa Bagamoyo, Tanzania.
KUHUSU TAMASHA:
Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ni tukio ambalo ni la kipekee na lenye kuvutia sana. Kwa kuwa linahusisha na kuchanganya aina mbalimbali za sanaa kama muziki wa asili na kisasa, ngoma, maigizo, sarakasi, vichekesho, mazingaombwe, mashairi, maonyesho (exhibition) na sanaa zingine. Tamasha hili linatoa jukwaa la kipekee kwa wasanii wa ndani na kimataifa kushirikiana na kubadilishana uzoefu na ujuzi.
SIFA ZA USHIRIKI:
TaSUBa inawakaribisha wasanii wa fani mbalimbali za sanaa na utamaduni kwa ajili ya kuomba kushiriki katika Tamasha. Iwe wewe ni mwimbaji, mwanamuziki, mchekeshaji, msanii wa sanaa za ufundi (mchoraji, mchonga sanamu), au mtaalamu mwingine wa ubunifu, tunakaribisha maombi yako ya kushiriki katika Tamasha.
JINSI YA KUOMBA NA MAELEKEZO MENGINE TAFADHALI PITA LINK ZIFUATAZO
WITO KWA WASANII
WITO KWA WASANII - Tamasha la Bagamoyo 2025.pdf
FOMU YA USHIRIKI
FOMU YA USHIRIKI WA TAMASHA - 2025.pdf
MAWASILIANO ZAIDI
Namba za Simu: +255(0) 755 853 436, +255(0) 714 510 386, and +255(0) 788 840 405
Barua Pepe: bagamoyofest@tasuba.ac.tz au bagamoyofest@gmail.com
Tovuti: www.tasuba.ac.tz
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.