SERIKALI imeipongeza Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kazi nzuri inayoonekana kwa kuboresha miundombinu na kuhakikisha inaendelea kutoa elimu ya sanaa kwa viwango vinavyokubalika.
Akizungumza alipofanya ziara katika Taasisi hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Suleiman Serera, alisema amefurahishwa na maendeleo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo na kwamba Serikali itaendelea kutoa uwezeshaji wa kutosha ili kuhakikisha Chuo hicho kinazidi kwenda kimataifa.
"Nimefurahishwa na maendeleo yanayofanywa na TaSUBa ili kuhakikisha inaendelea kuzalisha wasanii bora na malengo ya chuo yanafikiwa," alisema Dk. Serera.
Amesema TaSUBa ni Chuo cha Kimataifa viwango vyake vinaonekana hivyo wasanii wengi wa Tanzania wanaofanya vizuri Kimataifa ni zao TaSUBa.
Kwa upande wake Mkuu wa TaSUBa, Dk. Herbert Makoye alisema wamejipanga vyema kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri ikiwemo kuongeza idadi ya wanafunzi watakaowadahili kuanzia mwaka ujao wa masomo.
"Tumefurahishwa na ugeni wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yetu, tunaahidi kuendelea kufanya vizuri ikiwemo kudahili wanafunzi wengi zaidi kuanzia muhula ujao masomo," alisema.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.