Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Prof. Kitila Mkumbo imeipongeza Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kufanya ukarabati wa miundombinu na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia kama ilivyoelekezwa na Serikali.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Kitila Mkumbo ameyasema hayo wilayani Bagamoyo wakati Kamati hiyo ilipotembelea TaSUBa Machi 18, 2023 ili kukagua utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/22 pamoja na kuona shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Taasisi hiyo.
"Sekta ya Utamaduni na Sanaa inatoa ajira kwa watu wengi, ni vizuri tukaendelea kuwekeza na kuweka mazingira bora kwa Taasisi hii ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kutosha na ununuzi wa vifaa vya kisasa ili wadau wetu wapate mafunzo bora ya kuendeleza vipaji vyao," amesisitiza Mhe. Kitila.
Ameongeza kuwa ipo haja kwa Serikali kuiongezea Bajeti Taasisi hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi pamoja na kuiongezea vifaa zaidi vya kujifunzia na kufundishia.
Kwa upande wao Wajumbe wa Kamati hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo wametoa wito kwa wadau katika Sekta Binafsi hususani wasanii na wanufaika wa kazi za sanaa waendelee kujitokeza kuchangia maendeleo ya Taasisi hiyo kwa kujenga miundombinu na kutoa vifaa vya kufundishia na kujifunzia badala ya kuiachia Serikali peke yake.
Naye Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameieleza Kamati hiyo kuwa Serikali inaeendelea kuweka jitihada kuboresha miundombinu ya Taasisi hiyo na inaialika Sekta binafsi pamoja na wadau wa sanaa kushirikiana na Serikali katika kukiendeleza Chuo hicho muhimu katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni nchini.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.