Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul ameupongeza uongozi wa Taasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa usimamizi mzuri wa fedha zinazoletwa katika Taasisi hiyo kwa kuzitumia vyema kuendana na mahitaji ya taasisi ili kuifanya taasisi kufikia malengo yake.
Naibu Waziri Gekul ametoa pongezi hizo leo Desemba Mosi, 2022 akiwa ni mgeni rasmi katika mahafali ya 33 ya TaSUBa yaliyofanyika katika kampasi ya TaSUBa Bagamoyo mkoani Pwani na kusisitiza kuwa, taaluma ya utamaduni na sanaa inayotolewa chuoni hapo ni taaluma muhimu sana kwa maendeleo ya jamii yoyote duniani.
Mbali na hilo, pia ameipongeza TaSUBa kwa ongezeko kubwa la udahili wa Wanafunzi katika chuo hicho hata kufikia hatua ya kuweka historia ya kudahili idadi kubwa ya wanafunzi ambayo haijawahi kufikiwa tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo.
Kufuatia hilo naibu waziri Gekul amebainisha kuwa, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iliona wazi umuhimu wa taaluma hiyo na hivyo kuanzisha sera maalum kusimamia.
"TaSUBa ni taasisi ya pekee nchini kwetu na ukanda wa Afrika Mashariki inayotoa mafunzo ya sanaa kwa ngazi ya stashahada na astashahada hivyo basi kuna umuhimu mkubwa wa kuboresha taaluma hii ili iendane na mazingira ya sasa ya utandawazi"
Naibu Waziri huyo ameutaka uongozi wa TaSUBa kuendeleza ubunifu zaidi kwa kuanzisha kozi ambazo zitawavutia watu wengi kujiunga na chuo hicho.
Naye Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye amesema kuwa, kwa miaka mitatu mfululizo kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi chuoni hapo na hiyo ni kutokana na jitihada mbalimbali zilizochuliwa na serikali ya awamu ya sita, wadau pamoja na wao wenyewe kama taasisi.
Dkt. Makoye amezitaja miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na uamuzi wa serikali kuwapangia wahitimu wa kidato cha nne moja kwa moja kujiunga na chuo hicho pamoja na uhamishaji wa kila siku unaofanywa na TaSUBa pamoja na wadau wengine katika kukitangaza chuo hicho.
#TaSUBaKwaMafunzoBoraYaSanaaNaUtamaduni
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.Box 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 023 2440149
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2022 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.