WATU WA BAGAMOYO, LEO NDIO SIKU YA KILELE CHA TAMASHA LA 44 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO, 2026. Wananchi wa Mji wa Bagamoyo na Watanzania kwa ujumla wanahimizwa kujitokeza kwa wingi leo kushiriki katika kilele cha Tamasha la 44 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo 2026, linalohitimisha siku nne za maonesho na shughuli mbalimbali za sanaa na utamaduni.
Kilele cha tamasha hilo kinatarajiwa kuhudhuriwa na Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Shaibu Ndemanga, ambaye ataungana na wananchi pamoja na wadau mbalimbali katika kuhitimisha tamasha hilo.
Tamasha hili ni jukwaa muhimu la kukuza vipaji, kuenzi urithi wa kihistoria wa Bagamoyo na kuitangaza Tanzania kupitia sanaa, utamaduni na ubunifu.
WATU WA BAGAMOYO, HII NI SIKU YETU! Tujitokeze kwa wingi kuunga mkono sanaa na utamaduni wetu na kuifanya Bagamoyo iendelee kung'ara.
LEO NI KILELE! LEO NI BAGAMOYO!
#BagamoyoInternationalFestival2026 #TwenzetuBagamoyo #BagamoyoFestival
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.