TAMASHA la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo msimu wa 41, linatarajiwa kuzinduliwa Novemba 10, mwaka huu ambapo litakuwa Tamasha la siku tatu hadi Novemba 12, 2022.
Mgeni rasmi katika Tamasha hilo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Mhe. Dk. Philip Mpango ambaye atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza leo Bagamoyo na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbasi, amesema kwa kiasi kikubwa maandalizi hayo yamekamilika na litakuwa Tamasha la aina yake kwani litahusisha vikundi vya ndani na nje ya nchi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainabu Abdallah amewaondoa wasiwasi wageni pamoja na wote watakaohudhuria Tamasha hilo kuwa ulinzi na usalama utakua wa kiwango cha juu.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.