Waziri Bashungwa: Wizara Hii Sasa Ni Ya Moto, Tuchapekazi
Tamasha la 40 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni lilizinduliwa Oktoba 28, 2021, na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa katika viwanja vya TaSuBa mjini Bagamoyo.
Katika Tamasha hilo lilihudhuriwa na maelefu ya watu kutoka mikoa na maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi na kupata burudani kutoka wasaniii mbalimbali Waziri Bashungwa amesema ubunifu na nia ya kutaka sekta hizo za ubunifu kulisifia Taifa katika ajenda za maendeleo za Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan ndio nguzo kuu kwa sasa.
Wasanii kadhaa waliweza kuwakosha viongozi waliokuwepo ambapo walikuwepo mabalozi kutoka nchi za Japan, India, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Naibu Waziri wa Utamaduni, Pauline Gekul, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallah ambao mara kadhaa hawakusita kunyanyuka na kwenda kucheza.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.