Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wametakiwa kuendelea kuwa chachu ya mabadiliko kwa mtumishi mmoja mmoja na Taasisi kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo Novemba 07, 2024 na Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo Bi. Stella Msofe wakati akizindua Baraza la tatu la Wafanyakazi la Taasisi hiyo.
Bi. Msofe amesema Baraza la Wafanyakazi lipo kwa mujibu wa sheria hivyo mafanikio na ustawi wa TaSUBa lazima uletwe na wanabaraza.
Bi. Msofe amelitaka Baraza liwe la kutenda haki na lisiwe baraza la kuumiza wengine.
"Watumishi wanamatumaini makubwa na baraza hivyo baraza hili likalete utulivu kama mabaraza yaliyopita tusimuonee mtu wala tusimuumize mtu, baraza litoe maamuzi yanayobeba mustakabali wa jumuiya yote," amesema Bi. Msofe.
Aidha, Katibu Tawala Msofe amempongeza Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Herbert Makoye kwa kusimamia sheria na kusimamia uwepo wa Baraza la Wafanyakazi TaSUBa kwa kuhakikisha linaendelea kufanyika kila mwaka.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.