BODI ya Ushauri (MAB) ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imefanya kikao chake cha kwanza Julai 06, chini ya mwenyekiti wake Bw. George Yambesi ambaye ni Katibu Mkuu Mstaafu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Bw. Yambesi ametoa shukrani kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa kuwaamini na kuwateua kuwa wajumbe wa bodi hiyo.
“Tunamshukuru Waziri kwa uteuzi huu na tunaahidi kufanya kazi kwa weledi na nguvu zote ili kuleta tija na ufanisi katika kuijenga TaSUBa,” amesema Yambesi.
Vile vile Bw. Yambesi amemshukuru Mkuu wa Chuo Dkt. Herbert Makoye na menejimenti yote kwa mapokezi mazuri waliyowapa na kuahidi ushirikiano kwa uongozi wa chuo pamoja na wadau wengine wa sanaa.
Mwenyekiti Yambesi amewapongeza pia wajumbe wote wa bodi kwa kuteuliwa na kuwa sehemu katika mchango wa kuleta tija katika chuo hicho cha sanaa chenye ubora uliotukuka Afrika Mashariki katika kutoa mafunzo ya sanaa na utamaduni.
Naye Mkuu wa Chuo Dkt. Herbert Makoye kwa niaba ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, ameipongeza Bodi na kuwashukuru wajumbe kwa kukubali uteuzi huo.
“Menejimenti tuko tayari kufanya kazi na kutekeleza maelekezo ya bodi kwa kufanya kazi pamoja ili kufikia malengo yaliyofanya Serikali ifungue chuo hiki,” amesema Dkt. Makoye.
Wajumbe wa Bodi hiyo ambao ni Prof. Omary Halfa Mbura, Bw. Haruni Benge Matagane, Dkt. Elizabeth Godwin Mahenge na Dkt. Emmanuel Mwesiga Ishengoma, waliteuliwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa Machi 25, 2025.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.Box 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 023 2440149
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2022 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.