SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo itaendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ili kuendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kutokana na upekee wa Chuo hicho katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa katika Mahafali ya 35 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika Chuoni Bagamoyo Desemba 06, 2024.
Msigwa amesema TaSUBa ndio Chuo pekee kinacho toa mafunzo ya sanaa kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada hivyo kuwa na umuhimu mkubwa wa kuboresha zaidi taaluma inayotolewa Chuoni hapo ili iendane na kasi ya ukuaji wa matumizi ya teknolojia mpya katika uzalishaji wa kazi za sanaa hasa ugunduzi wa matumizi ya akili mnemba (AI)
“Nimeyasema hayo ili tuweze kuona namna Serikali ilivyojipanga kukifanya Chuo hiki kiweze kuzalisha wahitimu ambao tayari soko linawahitaji katika viwanda vya uzalishaji wa Sanaa ya Ubunifu,” amesema Msigwa.
Msigwa amesema ana matarajio makubwa kwa wahitimu kuwa, elimu waliyoipata itawasaidia kuingia kwenye tasnia ya sanaa na utamaduni wakiwa na mwelekeo wa sasa wa Serikali na Wizara wa kuzalisha ajira zaidi na kukuza biashara na uchumi kupitia kazi za sanaa.
“Kila mmoja wenu kwa nafasi yake anapaswa alijue hilo na abadilishe elimu na ujuzi alioupata ili kujiari na kuajiri wengine kufanya sanaa kwa mrengo wa biashara na kukuza uchumi wake na taifa kwa ujumla,” amesema Msigwa.
Katibu Mkuu Msigwa amewataka wahitimu na wasanii wote kuzingatia maadili ya Taifa hasa wanapozalisha kazi za sanaa na watambue kuwa wao ni kioo cha jamii.
Msigwa ameitaka TaSUBa kuendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi na kozi maalumu kwa wasanii na viongozi wa mashirikisho ya sanaa na vyama vya wasanii nchini ili kuendeleza vipaji vyao kwa pamoja.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.