SERIKALI imesema inataendelea kuiboresha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), ili kuhakikisha inatoa wasanii watakaoingia katika soko la ushindani kimataifa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma leo Machi 15, 2023 alifanya ziara kwa mara ya kwanza katika taasisi hiyo tangu alipoteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza mara baada ya kukagua Taasisi hiyo ikiwemo miundombinu, Naibu Waziri, Mwinjuma amesema kuwa serikali imejipanga kuiboresha taasisi hiyo ili kuhakikisha inatoa wasanii bora watakaoingia katika ushindani kimataifa.
Alisema lengo ni kuzalisha wasanii, watengeneza filamu, wanamuziki na wataalamu mbalimbali wa sekta ya sanaa ili kuendana na kasi iliyopo sokoni.
Mhe Naibu Waziri aliongeza kuwa amefurahia kufanya ziara TaSUBa kwa kuwa amekuwa katika tasnia ya sanaa na utamaduni kwa muda mrefu
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.