Naibu Waziri, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul ameipongeza Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutoa mafunzo na malezi katika kukuza taaluma ya sanaa na utamaduni ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya jamii yoyote duniani.
Mhe. Gekul ambae alikua mgeni rasmi katika mahafali ya 32 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) yaliyofanyika Disemba 17, 2021 katika ukumbi wa Taasisi ya Sanaa Bagamoyo, alisema Serikali inatambua umuhimu wa sanaa na utamaduni ndio maana kupitia wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeweka sera ya kusimamia utamaduni kwa ujumla na sanaa ikiwepo ndani yake.
“Taasisi hii ni ya pekee nchini mwetu na ukanda wa Afrika Mashariki inayotoa mafunzo ya sanaa kwa kiwango cha astashahada na stashahada, basi kuna umuhimu mkubwa wa kuboresha zaidi taaluma hii ili iendane na mazingira ya dunia ya sasa ya utandawazi,” alisema Mhe. Gekul.
Mhe. Naibu Waziri aliwashukuru wasanii (wanachuo) kwa maonyesho ya sanaa ikiwa ni sehemu ya shughuli muhimu zinazofanywa na Taasisi hiyo pamoja na wasanii wengine. “Hakika ni kazi nzuri zinazoonyesha umuhimu wa sanaa kwa maendeleo ya nchi yetu,” alisema Mhe. Gegul.
Mhe. Gekul amesema Serikali itashirikiana na wadau mbalimbali wa sanaa kuhakikisha TaSUBa inaendelea kua kituo bora cha mafunzo ya sanaa na utamaduni nchini na afrika kwa ujumla.
Jumla ya wahitimu waliotunukiwa vyeti ni 252 ambapo wahitimu wa Astashahada ni 150 (Me 118 na ke 32) na wa Stashahada ni 102 (Me 75 na ke 27).
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.