Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe. Dkt. Riziki Pembe Juma, ametaka kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, ili kupanua fursa za upatikanaji wa mafunzo ya sanaa na utamaduni kwa wananchi wa Zanzibar.
Mhe. Dkt. Riziki ameyasema hayo Novemba 16, 2026 wakati wa ziara yake TaSUBa, akiambatana na watendaji kutoka Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar.
Mhe. Dkt. Riziki amesema ushirikiano huo utasaidia kuweka utaratibu wa kutoa mafunzo ya sanaa na utamaduni Zanzibar kwa kutumia wataalamu na wakufunzi kutoka TaSUBa, hatua itakayopunguza gharama zinazowakabili wanafunzi wa Zanzibar wanaotamani kujiunga na TaSUBa lakini wanashindwa kutokana na gharama za kusafiri na kuishi Bagamoyo wakati wa masomo.
"Kupitia ushirikiano wetu, tunaweza kuwa na kozi ambazo wakufunzi wa TaSUBa watakuja kuzifundisha Zanzibar. Hii ni nafasi nzuri kwa TaSUBa kuwa na tawi,” amesema Mhe. Dkt. Riziki.
Aidha, amependekeza TaSUBa kuanzisha mfumo wa mafunzo kwa njia ya mtandao (Online Courses), utakaowezesha watu ambao hawana nafasi ya kufika chuoni kupata elimu na ujuzi katika fani mbalimbali za sanaa na utamaduni.
Amesema mfumo huo utakuwa fursa muhimu pia kwa wasanii wenye majina makubwa ambao wana nia ya kujiendeleza kielimu, lakini wanakabiliwa na changamoto ya kuhudhuria masomo chuoni kutokana na majukumu yao na mazingira yanayoambatana na umaarufu wao.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.