TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeingia makubaliano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ili kukuza, kuboresha na kutangaza Sanaa na Utamaduni wa mtanzania.
Akizungumza jana mjini Dodoma mara baada ya kusaini makubaliano hayo Hafla ya utiaji saini huo, imefanyika Dodoma tarehe 19 Juni, 2021 katika ofisi za TBC,Mkuu wa TaSUBa Dk. Herbert Makoye, alisema makubaliano hayo yataisaidia taasisi hiyo kutengeneza maudhui katika maeneo wanayoshughulikia.
Dk. Makoye alisema kupitia makubaliano hayo TBC watatengeneza vipindi vya runinga kwa njia ya tamthilia, hatua ambayo ni muhimu katika kufikisha ujumbe kwa wananchi.
Alisema kutengeneza tamthilia ni njia nzuri yakutangaza lugha ya Kiswahili na Utamaduni wa mtanzania.
Dk. Makoye aliongeza kuwa utengenezaji wa tamthilia utaisaidia TaSUBa kuonyesha kazi wanazofanya na mchango katika taifa na utamaduni.
"TaSUBa ina malengo ya kusaidia utamaduni wa mtanzania uvuke mipaka kwa kutumia vyombo vya habari vyenye nguvu ili kuzifikia ncho jirani wasifikiri sisi ni wa kupokea tu tamaduni zao"alisema.
Aidha, makubaliano hayo yatawapa nafasi wanafunzi TaSUBa kufanya mazoezi kwa vitendo wakiwa na uhitaji huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TBC Dk.Ayoub Rioba alimshukuru Mkuu wa TaSUBa kufuatia makubaliano hayo.
“TBC dhima yetu ni kuhakikisha kwamba tunaendeleza na kudumisha Utamaduni, kwa sababu utamaduni kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwa ni vyenzo muhimu katika kumuendeleza binadamu, taifa lisilo na utamaduni ni sawa na lililokufa” alisema.
Dk. Rioba alisema TBC wanatambua mchango wa TaSUBa katika kuendeleza utamaduni wa mtanzania.
Dkt. Rioba alisisitiza, “baada ya kusaini makubaliano haya kazi ya kuanza kuandaa kazi kazi za Sanaa itaanza mara moja ili zianze kuruka katika vyombo vyetu ambavyo ni redio, televisheni ambayo inaweza ikawa ni TBC1, TBC 2 na mitandao ya kijamii.”alisema.
Aidha Dk. Rioba aliongeza kuwa anaamini nia waliyonayo TaSUBa na TBC ni ya dhati na wote tunapenda kuona tunaendeleza Utamaduni wetu.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.