UJUMBE kutoka nchini Korea ya Kusini umetembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) leo April 26, 2023 na kuahidi kutoa mchango mkubwa katika kuiimarisha Taasisi hiyo hasa katika utoaji wa mafunzo ya filamu.
Korea ya Kusini kupitia Serikali ya Jiji la Busan imesaini makubaliano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo yakisimamiwa na Bodi ya Filamu Tanzania ili kuweza kusaidia kuimarisha Tasnia ya Filamu na kuanzisha Shule ya Filamu nchini (Film Academy).
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye amesema ushirikiano kati ya Korea ya Kusini na Tanzania utakua wa manufaa makubwa kwa Taasisi hiyo na Tasnia ya Filamu nchini kwa ujumla.
"Tuna uhakika wataalam watakuja kutoka Korea na watakuja pia kutusaidia kufundisha vijana wetu hapa TaSUBa," amesema Dkt. Makoye.
Dkt. Makoye ametoa wito kwa wadau wa tasnia ya filamu nchini kujiandaa kwa ajili ya fursa za mafunzo mara zitakapotokea ili kupata ujuzi zaidi na utaalam kutoka kwa wabobezi hawa kwa sababu ina tija kubwa katika tasnia hasa katika utengenezaji wa filamu zilizo na ubora unaokubalika na zenye ushindani katika soko la ndani la nje ya nchi.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.