Wanafunzi katoka Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) wakiambatana na Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo hicho, Taaluma, Utafiti na Ushauri pamoja na wakufunzi, wametembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Mei 25, 2022 ikiwa ni ziara ya kimasomo ili kutimiza matakwa ya makubaliano (MoU) kati ya vyuo hivyo viwili.
Katika ziara hiyo Kaimu Mkuu wa chuo TaSUBa, ambaye ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Mwl. Gabriel Kiiza alisema, makubaliano ambayo TaSUBa iliingia na TCTA yanahusisha utoaji wa mafunzo kwa kipindi cha muda mfupi kisichopungua mwezi mmoja na kisichozidi miezi mitatu kwa kila udhahili.
Mwl. Kiiza alisema, tasnia ya sanaa na utamaduni inahitaji ubunifu ili kuiboresha na kuleta vitu vipya kila wakati, ambapo mbali na kuwa ni burudani, ni sehemu ya ajira rasmi ambayo inahusisha kundi kubwa la vijana ambao ni nguvu kazi katika uchumi endelevu.
Kwa upande wake Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo TCTA Mrakibu wa Magereza Lihuwi Said Ngonya, alisema makubaliano hayo yamekuwa na tija kwa wanafunzi wa TCTA kwani wamepata na fursa ya kutembelea TaSUBa na kujifunza mengi.
Mrakibu Ngonya alisema, ushirikiano huo ni fursa nzuri ya kupeana uzoefu katika Sanaa na Utamaduni kwa kuwa TaSUBa wamebobea na wana uzoefu katika utoaji wa mafunzo hayo.
Makubaliano hayo kati ya TaSUBa na TCTA yanahitaji wanafunzi kutoka TCTA kutembelea TaSUBa ili kujifunza mazingira ya Taasisi hiyo kabla ya kuhitimu mafunzo angalau mara moja kwa kila udhahili.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.