Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa,amezitakaa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo hasa Taasisi ya Sanaa naUtamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kujiepusha na masula ya Rushwa, Uvivu, ubadhirifuna upendeleo kwenye tasnia ya sanaa ili kuweza kukuza sanaa nchini iliitambulike kimataifa.
Ameyasema hayo alipotembelea Taasisi ya Sanaa na UtamaduniBagamoyo (TaSUBa) Februari 09, 2022 na kuona mikakati inayoendelea kufanyikakatika Taasisi hiyo na kuitaja kuwa ni Taasisi ya kimkakati kwa Taifa. AidhaWaziri Mchengerwa ameahidi mageuzi makubwa ndani ya Taasisi hiyo hukuakitoa jukumu la kushirikiana na wadau kufanya utafiti wa falsafa ya muziki waTanzania (Tanzanian sound/beat).
Mchengerwa amesema kulingana na kauli ya Rais Mhe. Samia SuluhuHassan kuhusu kutafuta vijana wenye vipaji katika sanaa mtaa kwa mtaa,anategemea TaSUBa kusaidia kuwabaini vijana wenye vipaji na kuwasaidia.
Amesema Wizara inajipanga kuhakikisha Taasisi hiyo inakuwa naTelevisheni yake ambayo kukiwa na matamasha ya Utamaduni na Sanaa au matangazombalimbali yanayohusu sanaa yawe yanarushwa moja kwa moja kwenye televishenihiyo.
Hata hivyo amesema suala la Rushwa, uzembe na upendeleoataendelea kupiga vita kwa maana yanashusha thamani na kuturudisha nyuma kamataifa, kila jambo linawezekana tunaweza tukashiriki mashindano makubwa yakimataifa kama tutaamua. Pamoja na hayo Mchengerwa amesema wapo katika mkakatiwa kunzisha shule za michezo nchini ambazo zitakuwa daraja la kuinua vipaji vyamichezo kwa vijana wa kitanzania mbao wapo mtaani.
"Tumekubaliana na watendaji kwamba tunakwendakuanzisha shule 56 za michezo nchini ambapo shule moja itakuwa hapa Bagamoyokwasababu ya mazingira lakini tutajipanga namna ya kufanya ili kuboresha baadhiya viwanja vyetu ikiwemo kiwanja cha Mwanakalengwe kilichopo wilayaniBagamoyo".
Katika ziara hiyo Waziri Mchengerwa aliambatana na Katibu Mkuu,Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Mhe. Said Yakub pamoja na Mkuu wa Wilayaya Bagamoyo Mhe. Zainab Abdallah.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.