Historia ya Main Theater ya TaSUBa, kutoka jengo la makuti hadi ukumbi wa kisasa
Mkufunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), John Sagatti, ameeleza historia ya Jukwaa Kubwa la TaSUBa (Main Theater), akibainisha kuwa lilijengwa kwa mara ya kwanza mwaka 1990 wakati akiwa mwanafunzi wa taasisi hiyo.
Sagatti amesema ukumbi huo wa awali ulijengwa kwa kutumia makuti, lakini baadaye uliungua moto. Mwaka 2007, ukumbi huo ulijengwa upya kwa muundo na vifaa tofauti vya ujenzi, kupitia ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali za Norway na Sweden.
Ameeleza kuwa tangu wakati huo, ukumbi huo umeendelea kutumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo mafunzo, maonesho ya sanaa, mazoezi ya wanafunzi wa programu mbalimbali, mikutano ya dini, vyama vya siasa pamoja na mikutano ya hadhara na ya ndani.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.