Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo imekuja na nguvu kubwa ili kuleta maboresho na mabadiliko ya kisasa katika ukuaji wa Sekta ya Filamu nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Mohammedi Mchengerwa alipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) April 09, 2022.
Mhe. Waziri ambaye aliongozana Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Said Yakubu, pamoja na viongozi kutoka Kampuni ya Nichani ya India ikiongozwa na Bw. Manu Nichani na Trans Innova ya Marekani ikiongozwa na Dkt. David Faria, amesema lengo la kuja kwa viongozi hao ni kuona namna gani wanaweza kutusaidia kufanya mabadiliko ya pamoja na kupata uzoefu katika sekta ya filamu.
“Dhamira ya Serikali ni kuleta mapinduzi ya dhati katika Sekta ya Filamu na tumedhamiria kweli kweli kuitoa hapa ilipo na kuipeleka mbele zaidi,” alisema Mhe. Mchengerwa.
Mhe. Waziri amesema Wizara kupitia mashirikiano baina ya Kampuni hizo mbili itafanya mambo makubwa ambayo watanzania watayafurahia na yatadumu kwa kizazi cha leo na cha baadae.
Mhe. Waziri amesema, wataalam hao wanampango wa kukutana wa waigizaji wa filamu nchini ili nao wapate uzoefu wa namna ya kuzalisha filamu na tamthilia.
“Wenzetu hawa wametupa uhakika wa kutusaidia katika kupata masoko, kutangaza kazi zetu na kuzifanya ziwe za kimataifa zaidi, amesema Mhe. Mchengerwa.
Mhe. Mchengerwa amesema ziara hio ilikua muhimu kwasababu itakua na manufaa kwetu ili wenzetu hao waweze kutusaidia kutuvusha hapa tulipo na kwenda mbele zaidi.
Mhe. Waziri amesema kama nchi tunataka tuwe miongoni mwa mataifa ambayo yako mbele zaidi katika kuandaa filamu.
“Tutaendelea kuwatia moyo waandaaji wa filamu, waigizaji na wazalishaji wa filamu, lakini pia wanunuzi wa filamu ili kwa pamoja tuweze kufanikisha wazo na maono ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kuhakikisha Wizara hii inaleta furaha na faraja kwa Watanzania,” amesema Mhe. Waziri.
Naye Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye amesema TaSUBa inapata nguvu kubwa ya kusonga mbele kutokana na ushirikiano na uwezeshwaji mkubwa ambao Chuo kinapata kutoka kwa Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.