Mfumo wa e-Mrejesho umeendelea kurahisisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi kwa kuwawezesha wananchi na wadau kutoa maoni, kuuliza maswali, kuwasilisha malalamiko na pongezi pamoja na kupata majibu kwa haraka zaidi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Savera Salvatory, tarehe 9 Juni, 2026, Mtumba jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya Mfumo wa e-Mrejesho kwa waratibu wa mfumo huo kutoka Wizara na taasisi zake.
Bi. Savera amesema kuwa mfumo huo unawapa wananchi fursa ya kuwasilisha maoni, mapendekezo, pongezi na malalamiko kuhusu huduma wanazopata kutoka katika Wizara na taasisi zake, hivyo kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utoaji wa huduma za umma.
“Kupitia mfumo huu, taarifa zimekuwa zikipokelewa na kufanyiwa kazi kwa wakati, huku wananchi wakipatiwa mrejesho popote walipo bila kulazimika kufika katika ofisi za Wizara,” amesisitiza Bi. Savera.
Aidha, amewataka washiriki wa mafunzo hayo, ambao ni Maafisa Habari, Maafisa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Maafisa TEHAMA, kuhakikisha wanatumia ujuzi watakaoupata kuimarisha zaidi Dawati la e-Mrejesho ili huduma hiyo iwafikie wananchi wengi zaidi.
Mafunzo hayo yanatolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, ambapo, waratibu wa mfumo huo taasisi za wizara wameshiriki.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.