MKUFUNZI katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Bi. Beatrice Taisamo, amesema kuwa nidhamu katika kazi ni moja ya nguzo muhimu zinazo mwezesha msanii kukua kitaaluma na kuzalisha kazi zenye ubora unaokubalika.Akizungumza kuhusu safari yake ya sanaa, Bi. Taisamo alieleza kuwa msanii mwenye nidhamu huipa kazi yake muda, heshima na nguvu zote zinazohitajika ili kufikia malengo aliyojiwekea. Anaongeza kuwa nidhamu humsaidia msanii kushirikiana vyema na wenzake, jambo ambalo huongeza ufanisi na mafanikio katika kazi za pamoja.Bi. Taisamo pia alibainisha kuwa aliamua kujiunga na TaSUBa kwa lengo la kunoa na kukuza kipaji chake cha uigizaji baada ya kugundua kuwa alikuwa na uwezo mkubwa katika sanaa hiyo. Kupitia mafunzo aliyoyapata chuoni hapo, ameweza kuimarisha ujuzi wake na hatimaye kuwa miongoni mwa walimu wanaochangia kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii chipukizi nchini.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.