Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeingia makubaliano ya ushirikiano katika kuendesha Mafunzo ya Kozi za Sanaa na Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA).
Makubaliano hayo ambayo yamesainiwa Ukonga katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania na wakuu wa Taasisi hizo mbili ambao ni Bw. Gabriel Kiiza, Kaimu Mkuu wa Chuo TaSUBa na Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani, Mkuu wa Chuo TCTA, wamekubaliana kwamba TaSUBa kwa kushirikiana na TCTA wataandaa na kutoa mafunzo ya kozi za sanaa katika maeneo ya muziki, uigizaji na Ngoma; pia mafunzo yatakuwa yanatolewa kwa kipindi cha muda mfupi (Short Courses) kwa kipindi kisichopungua mwezi moja na kisichozidi miezi mitatu kwa kila udhahili. Aidha mafunzo yatatolewa na kuendeshwa katika madarasa ya TCTA ambapo maktaba pamoja na vifaa vya kujifunzia vitakuwa vya TCTA na endapo TCTA itakuwa na uhaba wa vifaa vya mafunzo, vitaazimwa kutoka TaSUBa kama vitakwepo vyakutosheleza.
Vile vile, bila kuathiri Ibara ya 3(a) ya Makubaliano hayo, TCTA itakuwa na wajibu wa kuwasafirisha wanafunzi na kuwapeleka TaSUBa kabla ya kuhitimu mafunzo angalau mara moja kwa kila udhahili ili kuweza kujifunza mazingira ya TaSUBa.
Awali kabla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Mkuu wa Chuo TCTA, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joe Gideon Matani alisema, utiaji saini wa makubaliano hayo lilikua jambo la maandalizi la muda mrefu lakini sasa anafarijika kwa kuwa limekamilika na sasa kazi iendelee.
Mashirikiano hayo yatakua ni fursa nzuri ya kupeana uzoefu katika mafunzo hayo ya Sanaa na Utamaduni kwa kuwa TaSUBa wamebobea na wana uzoefu katika utoaji wa mafunzo ya Sanaa na Utamaduni kwa miaka mingi.
Awali chuo hicho kilikua kikitoa mafunzo kwa askari tu lakini sasa wamepanua wigo na kinatoa mafunzo kwa askari na raia.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.