• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • NeST |
    • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS)) |
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)
TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Huduma Zetu
    • Kikundi cha Bagamoyo
    • Vyumba vya Mikutano
    • Ushauri
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Ofisi
    • Vitengo
  • Taaluma
    • Kozi Zitolewazo
    • Fomu za Maombi
    • Matokeo ya Mtihani
    • Prospectus
  • Tamasha la Bagamoyo
    • Tamasha la 44
    • Tamasha la 43
    • Tamasha la 42
    • Tamasha la 41
    • Tamasha la 40
    • Tamasha la 39
    • Tamasha la 38
  • Kituo cha habari
    • TaSUBa TV
    • Maktaba ya Picha
  • Wasiliana
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Majarida
    • Vipeperushi
    • Taarifa kwa umma

*WAFANYABIASHARA KUNUFAIKA NA TAMASHA LA 43 LA BAGAMOYO*

Posted on: October 22nd, 2024

Wafanyabiashara na wajasiriamali wa sanaa za ufundi wanatarajiwa kunufaika na Tamasha la 43 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku Nne Mfululizo katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Mkoani Pwani kuanzia Oktoba 23 hadi 26, 2024.

Akizungumza na waandishi wa Habari Bagamoyo Mkoani Pwani Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa lengo la Tamasha halitakuwa ni Kuitangaza Bagamoyo pekee bali Nchi nzima na Afrika Mashariki.

Amesema Wafanyabishara hao wataweza kuonesha na kuuza bidhaa zao kitaifa na kimataifa ikiwemo Batiki, Shanga Magauni, Hereni, vikapu Ngoma, picha Michoro ,Mashati, Virutubisho na Tibalishe.

Tamasha hilo ambalo litazinduliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro linalenga kuvutia Wadau wa Nje na Ndani ya Nchi ambapo pia litahusha shughuli za kisanii, Kiutalii, kijamii na Kiuchumi.

Pia, Amesisitiza Kuwa Maandalizi ni mazuri  na tayari kwa ajili ya kupokea wageni kutoka Mataifa mbalimbali Duniani huku burudani bora zaidi zikitarajiwa kulinganisha matamasha mengine yaliyowahi kufanyika.

Aidha, Mhe. Mwinjuma Amesema kuwa Lengo la sasa ni kuhakikisha wanafikia Tamasha la siku saba tofauti na ilivyo sasa la siku nne ili kusaidia vivutio vyote vya Utalii  vilivyopo bagamoyo  vinajulikana Dunia nzima

Naye Mkuu wa Taasisi ya Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye ameeleza Kuwa Tamasha hilo linatarajiwa  kuhudhiriwa na Viongizi wa serikali, Makampuni Binafsi, Vyama vya siasa na Viongozi wa Dini mbalimbali.

Dkt. Makoye amesema pia Tamsha hili litahusisha Vikundi 74 ambapo  vikundi 61 ni kutoka Tanzania Bara,  2 kutoka Zanzibar na 11  vya kimataifa kutoka Afrika Kusini Zambia, India, Ujerumani, Brazili Hispania,  Botswana, na Visiwa vya Mayotem (Ufaransa).

Vikundi hivyo vitafanya maonesho Jukwani ikiwemo Ngoma za Asili, Mziki wa Asili na wa kisasa Maigizo, Sarakasi, Vichekesho na Mazingaombwe.

Aidha, Tamasha hili litatanguliwa na Mkesha maalumu utakaofanywa usiku wa leo Jumanne tarehe 22 kuamkia Jumatano ya tarehe 23 Oktoba 2024.

Matangazo

  • FEES STRUCTURE FOR ACADEMIC YEAR 2026-2027 June 03, 2026
  • FOMU YA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2026-2027 September intake June 03, 2026
  • Join instruction for TAMISEMI 2026-2027 June 03, 2026
  • majina ya waombaji ambao wamechaguliwa na NACTVET kujiunga na Taasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo ingizo la Septemba 2025 August 15, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ELIMU NA MAZOEZI SIRI YA MAFANIKIO KATIKA SANAA YA UCHORAJI

    June 25, 2026
  • KARIBU TaSUBa KWA MWAKA WA MASOMO 2026/2027

    June 25, 2026
  • CALL FOR ARTISTS TO PARTICIPATE IN THE 44th EDITION OF THE BAGAMOYO INTERNATIONAL FESTIVAL OF ARTS AND CULTURE

    June 23, 2026
  • NIDHAMU NI MSINGI WA MAFANIKIO KWA MSANII

    June 22, 2026
  • Angalia zote

Video

ELIMU NA MAZOEZI SIRI YA MAFANIKIO KATIKA SANAA YA UCHORAJI
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dirisha la Watumishi (Employee Self Service (ESS))
  • Dirisha la Hati ya Mshahara
  • Baraza la Sanaa la Taifa

Viunganishi Linganifu

  • WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Kaole Road

    Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania

    Simu: +255 762544613

    Simu ya kiganjani: +255 766 264 581

    Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas

Other Contacts

   

Idadi ya waliotembelea Tovuti

Counter Widgets

    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.