Wanachuo wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wamepata semina maalum iliyotolewa na Rais Mstaafu wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Eliya Mjatta, iliyolenga kuwajengea uwezo wa kubadili vipaji vyao vya kisanaa kuwa chanzo endelevu cha kipato na maendeleo ya kiuchumi.Akizungumza katika semina hiyo, mwezeshaji huyo aliwahimiza wanafunzi kuondokana na mtazamo wa kuona sanaa kama kipaji pekee na badala yake kuichukulia kama biashara yenye uwezo wa kuzalisha ajira, kipato na fursa mbalimbali za maendeleo.Alieleza kuwa mafanikio katika sekta ya sanaa yanahitaji ubunifu unaoambatana na fikra za kibiashara, ikiwa ni pamoja na kutambua mahitaji ya soko, kujitangaza kitaalamu, kujenga mitandao ya kikazi na kuwekeza katika ujuzi unaoongeza thamani ya kazi zao.
Kaole Road
Anuani ya posta: P.O.BOX 32 Bagamoyo Tanzania
Simu: +255 762544613
Simu ya kiganjani: +255 766 264 581
Barua pepe: application@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu masomo) info@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo ya ujumla) bagamoyofest@tasuba.ac.tz (Barua pepe hii inatumika kwenye mambo yote yanayohusu Tamasha) tas
Copyright ©2024 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) . All rights reserved.